NYOTA YA MIZANI (LIBRA)
Hii ni nyota ya saba katika mlolongo wa nyota 12
Sayari yako ni VENUS (ZUHURA).
Siku yako ya Bahati ni Ijumaa.
Namba ya Bahati ni 6.
Rangi ya Bahati ni Kijani isiyoiva.
Asili ya nyota hii ni Hewa.
KIPAJI CHA MIZANI
(Extra Sensory Perception)
Wenye nyota hii wana kipaji cha kufumbua mafumbo na kujua siri za watu bila kuambiwa.
TABIA ZA MIZANI:
Wenye nyota ya Mizani wana tabia ya kupenda usuluhishi, amani na upatanishi. Ni watu wasikivu, watiifu, na wepesi kuongozwa. Ni wenye maumbo ya kupendeza hasa wanawake. Kwa ujumla ni watu wenye roho nzuri na wanajua kupenda na wenye mahaba mengi.
Ni watu wastraabu, wenye adabu heshima na ni wakarimu kwa mtu yeyote na wanajipenda sana. Katika maisha yao wajipenda sana.
TABIA YA MIZANI KATIKA MAPENZI
Kujihusisha na suala la mapenzi kwa wenye nyota hii ni kitu cha kawaida kabisa pamoja na kwamba wenye nyota hii wanachukua muda mrefu kufanya maamuzi na inawawia vigumu sana kuchagua kati ya wapenzi wawili yupi anaefaa. Kwao kuishi vizuri ni kuwa na mpenzi au uhusiano wa kimapenzi.
Watu wa mizani wanathamini sana mapenzi kuliko hata maisha yao wenyewe na wanapenda sana kujionyesha kwamba wanapendwa.
Kwa sababu hizo wengi sana wanapumbazwa na mapenzi na ndoa zao zinakuwa zina
matatizo na zisizo na raha kwa sababu ya kuoa mapema bila kuangalia. Wenye nyota hii wanaonelea bora kuishi katika ndoa yenye matatizo kuliko kuishi peke yao.
Katika suala la mahaba (Romance) na ngono (Sex) wao ni mabingwa. Wanajua sana
kumpendeza mwanamke kwa maneno matamu yenye mpangilio na zawadi za thamani na wawapo kitandani wanatumia muda mrefu kuwachezea wapenzi wao sehemu nyeti.
Kwa ujumla wenye nyota ya Mizani wanapenda kuishi vizuri na wanapenda wapenzi wao nao waishi katika hali nzuri
MADINI YA MIZANI
Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa LAPIS LAZULI. Mawe kama nye rangi ya Bluu iliyokoza, wamisri wanayaita mawe ya peponi. Yakiwekwa kama kito kwenye pete ya dhahabu yanaleta mizani kwa wenye nyota hii.
UHUSIANO WA KIMAPENZI
(Punda na Mizani)
Tabia ya Punda ya haraka haraka. Vishindo na kutumia nguvu bila kufikiria, hulainishwa au kuzimwa na diplomasia, uerevu na ujanja wa mizani. Punda vile vile hupendezwa na uwezo au kipaji cha mahaba walichonacho wenye nyota ya mizani
pAmoja sana mtalam
ReplyDeletebhana mm umenipatia sana
ReplyDeleteNikweli
DeleteAsante sana umenipatia
ReplyDeleteMi naitw steven nimezaliw tareh 4/3 nyota yang natak niijue
ReplyDeleteWatu wa mizani na copper wanahusiana vipi
ReplyDeleteNa wenye nyota ya mizani wanatakiwa wawe na wachumba wa majina ya Aina gni au wa dezine gani na nyota inahusiana nini haswa na Maisha ya mtu binafsi
ReplyDeleteHizo namba za bahati zinamaanisha nini Kwa muhusika
ReplyDeletemm nimezaliw 23 october nataka kujitambua
ReplyDeleteYaan kuna nyingne unacalculate jina lako na la mama nyingne ni miez zpo tofauti y
ReplyDeleteVizuri hii ni nyoote yangu pia
ReplyDeleteMm nimezaliwa tarehe 8/1/ nataka kufahamu nyota yangu
ReplyDeleteNakubali mko pouwa saana
ReplyDeleteKweli kabsa
ReplyDeleteKweli kabsa
ReplyDeleteTrue
ReplyDeleteNyota yangu namba saba mizani na nasomea sharia now
ReplyDeleteTrue
ReplyDeletePoa
ReplyDelete